MAAJABU:SHULE ILIYOPO MITA 800 KWENYE BONDE

Wanafunzi kadha wa shule moja eneo la Sichuan, China wamepata ngazi mpya kuwasaidia kupanda na kushuka urefu wa mita 800 kufika na kuondoka shuleni.

Kijiji cha Atuler kimepewa jina la utani "kijiji cha mwamba". Kijiji hiki hupatikana mita 800 juu kwenye nyika eneo la Sichuan, China. Wanaoishi hapa ni watu wa jamii ya Yi, ambao pia hupatikana Vietnam na Thailand

Hadi kufikia sasa, kulikuwa na ngazi 17 za mbao ambayo ilikuwa njia pekee ya wakazi wa kijiji hiki kutoka nje ya kijiji chao. Kupanda ngazi hizi lilikuwa jambo hatari na watu zaidi ya saba walifariki wakizikwea, wakazi wanasema.

Watoto karibu 20 kutoka kijiji cha Atuler husomea shule ya bweni, na ndipo waweze kufika hutakiwa kushuka kwa kutumia ngazi hiyo. Wakati wa likizo, shule zinapofungwa, hutakiwa kupanda ngazi tena kurejea kijijini.

Sasa, ngazi ya chuma imejengwa kurahisisha safari yao. Lakini bado ni shughuli hatari, ingawa muda wanaotumia kupanda na kushuka umepungua

Sasa, ngazi ya chuma imejengwa kurahisisha safari yao. Lakini bado ni shughuli hatari, ingawa muda wanaotumia kupanda na kushuka umepungua

Watu wa jamii ya Yi wanaoishi Atuler wamekuwa wakikwea mwamba huo kwa miaka na mikaka na wana hata kanuni za kupanda. Wakati wa kupanda, wanaume wanawajibika kuwabeba na kuwatunza watoto. Watoto wa chini ya miaka 16 hawaruhusiwi kupanda au kushuka kwenye ngazi hiyo wakiwa peke yao.

MAAJABU:SHULE ILIYOPO MITA 800 KWENYE BONDE MAAJABU:SHULE ILIYOPO MITA 800 KWENYE BONDE Reviewed by teamcruisergenuineparts on 21:49 Rating: 5

No comments:

Home Ads

Powered by Blogger.