KIUNGO wa Manchester United, Ander Herrera amempiku mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na winga Antonio Valencia na kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa klabu katika sherehe za tuzo zilizofanyika Uwanja wa Old Trafford Alhamisi usiku.
Kwa kura zilizopigwa na mashabiki hakukuwa na mshindi kabisa, kwani wachezaji wawili wa juu walitenganishwa na kura 20 hadi saa za mwisho za upigaji kura kwa mujibu wa tovuti ya Manchester United
Lakini Herrera akafanikiwa kuibuka mshindi baada ya kazi nzuri aliyoifanya katika kiungo msimu huu, huku Valencia akitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Wachezaji wa Mwaka kama kupata suluhu, huku Ibrahimovic akiondoka mikono mitupu licha ya kuwa na msimu mzuri pia.
Herrera alisema: "Ni maalum sana kwangu kushinda tuzo hii, kwa sababu ukiona orodha ya washindi unaona ni muhimu kiasi gani...na kwa sababu nimezuia rekodi ya David [de Gea] na kwa vizuri zaidi kwa sababu tuzo inabaki Hispania,".
Bao LA msimu Antonio Valencia...
Mchezaji chipukizi Henrikh Mkhitaryan
Mchezaji Bora wa Timu ya Wachezaji wa akiba...Axel tuanzebe
mchezaji chipukizi: Angel Gomes
No comments: